Mimi ni mtoto wa mwisho kati ya watoto sita ambapo wa kwanza ni Leticia, akifatiwa na James, Tabu,Suzzy na Edward.
Nimezaliwa katika Jiombo la Nyamagana jijini Mwanza, baba yangu anaitwa Mzee Lutonja Simbitti mzaliwa wa Jimbo la Kwimba jijini Mwanza na mama yangu ni Prisca Juma Mzaliwa wa Nyamagana Mwanza, nawapenda sana wazazi wangu.
Nilipata elimu yangu ya Msingi katika shule ya Ngasamo iliyoko Magu-Mwanza na baada ya kuhitimu shule ya msingi nilijiunga na Sekondari ya Bulima iliyoko Magu-Mwanza ambapo nilisoma mpaka kidato cha nne na baabae nikajiunga na Sekondari Jamhuri iliyoko Dodoma ambapo nilisoma kidato cha tano na sita.
Baadae nikajiunga na Royal College of Tanzania nikichukua fani ya Utangazaji na Uandishi wa habari.Malengo yangu ni kuwa Mwanaharaki wa kutetea haki za binadamu, kuwa rais wa Tanzania nchi yangu ili niwakomboe wanaoonewa, pia napenda kusoma sana ndio maana mpaka sasa niko chuo ila sikuambii ni wapi, ninapendezwa sana falsafa za Lenin,Josef Stalen, Dk.karl Marx,Mwalimu JK Nyerere pamoja na Yesu Krito, hakika hawa watu walikuwa wapigania haki,zaidi na mimi ninapenda kuwa hivyo ndoto zangu zinaelekea ninakotaka.